Hawa ndiyo viumbe hatari zaidi kwa mwanadamu kote duniani

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:36 AM Oct 01 2024
Hawa ndiyo viumbe hatari zaidi  kwa mwanadamu kote duniani
Picha:Mtandao
Hawa ndiyo viumbe hatari zaidi kwa mwanadamu kote duniani

WENGI wanaweza kuwaza kuwa ni simba na mamba, au chui ama tembo lakini, wanyama wengi hawana hatari kuliko inavyotarajia. Mfano papa, huua wanadamu 70 kila mwaka.

Inashangaza kwamba viumbe hatari zaidi duniani mara nyingi ni vidogo zaidi lakini vina uwezekano mkubwa wa kuua kwa magonjwa na sumu badala ya meno yenye ncha kali. 

Mfano virusi kama vya homa ya ini, ebola na Corona ni vitu vinavyotisha ila havina meno wala ukubwa wa mwili. 

Kiumbe hatari au namba moja kwa mauaji ni mbu huua watu takribani 725,000 kwa mwaka. Ndiye mdudu hatari zaidi duniani huangamiza wazee kwa vijana kupitia magonjwa yanayoeneza kama vile malaria. Mbu jike pekee anauma na kuleta hatari zaidi.

Kupitia uwezo wao wa juu wa kuua, mdudu huyu mdogo anayeruka ameongoza kuua wanadamu na kwa miaka mingi. Maambukizi ya malaria ni hatari Afrika, huku eneo hilo likiwa na asilimia 95 ya wagonjwa na asilimia 96 ya vifo kote duniani.

BINADAMU WAMO 

Wanadamu husababisha vifo 400,000 kwa mwaka. Ni wanyama wa pili hatari zaidi duniani linapokuja suala la vifo vya watu. Japo ndiye anayehesabu mauaji. Ndiye anayeua zaidi pia.

Asilimia 0.7 ya vifo mwaka 2019 vilitokana na mauaji.  Amerika ya Kusini, viwango vya mauaji ni vya juu zaidi kuliko sehemu nyingine zozote duniani na mauaji yanachangia zaidi ya asilimia saba  ya vifo nchini El Salvador.

Wanadamu hawako peke yao katika kuuana wenyewe. 

Ni bora kuepuka mbu iwezekanavyo kwa kununua na kufunga chandarua ikiwa unapanga kusafiri katika maeneo ambayo wadudu ni tatizo, unaweza kujikinga pia lakini si kwa binadamu.

Nyoka wamo huua watu 138,000 kwa mwaka, lakini ni nyoka wa aina gani?

Nyoka hatari wanaweza kupatikana duniani kote na wanaweza kuua wanadamu kwa njia tofauti na za kikatili. Mfano koboko (black mamba), anaweza kuua binadamu kwa matone mawili ya sumu ilhali chatu wanaweza kummeza mtu mzima.

Chatu hushambulia kwa kuzungusha miili yao mirefu kuzunguka na kubana mawindo yao, na kuwakosesha pumzi na kuvunja mifupa hasa mbavu.

Kisha hutumia taya zilizonyooshwa kumeza. Ndiyo, wanakua wakubwa vya kutosha kumeza mtu mzima, na chatu wanaojulikana hukua hadi mita 10 kwa urefu.

Wengi wanamfahamu kunguni kwa harufu mbaya lakini ni  hatari anasababisha ugonjwa wa chagas, unaoua watu 100,000 kwa mwaka.

Pia wapo mbwa wenye kichaa wakiwaua watu  59,000 kwa mwaka. Japo ni rafiki bora wa mwanadamu anaweza kuwa adui mbaya zaidi wa mtu linapokuja suala la kichaa cha mbwa.

Mbwa wanapenda kuwalinda wamiliki wao dhidi ya wavamizi na watashambulia kwa kuuma. Wakati vifo vinavyotokana na kushambuliwa na mbwa si vya kawaida, mauaji ya binadamu kutokana na kichaa cha mbwa kinachoenezwa kwa kuumwa na mbwa si jambo la kawaida kusikika.

Vifo vinatokea katika sehemu wanapoishi maskini zaidi za dunia ikiwa ni pamoja na Afrika na Asia.

Shirika la Afya Duniani (WHO),  linasema :“Mbwa ndio chanzo kikuu cha vifo vitokanavyo na kichaa na hivyo kuchangia hadi asilimia 99 ya maambukizi yote ya kichaa cha mbwa kwa wanadamu.”

Kichaa huambukizwa kwa mate kupitia kuumwa, mikwaruzo na kugusa moja kwa moja na maeneo yaliyoambukizwa kwenye mbwa.

Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, nge naye yupo  anayewaua watu 3,300 kwa mwaka.

Wadudu hawa wa kale watambao na wakali huuma na mkia wao na kuingiza sumu kwenye mawindo yao. Pamoja na kuwapo zaidi ya spishi 2,600, karibu 25 pekee hubeba sumu yenye nguvu ya kutosha kuua wanadamu.

Sumu huua vijana, wazee na wale walio na matatizo ya kiafya yanayoendelea ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo. Binadamu wazima wenye afya njema wanaweza kuuawa kwa kuumwa pia hasa nchi za Amerika ya Kusini. 

Mamba  nao wamo  huua watu 1,000. Ni mnyama mkali ambaye husababisha hadi vifo 1,000 vinavyoripotiwa kwa mwaka. Kumuangalia  meno kunapaswa kukuambia kwa nini wanyama hawa watambaao ni hatari.

Mfano mamba wa Mto Nile ana nguvu ya kuuma zaidi ana nguvu zaidi kuliko mnyama yeyote duniani, huku mamba wa maji ya chumvi akiwa na nguvu kidogo.

Mamba ni wakali na hushambulia kitu chochote kinachoingia kwenye makazi yao, mara nyingi huvizia mawindo wakiwa majini.

Tembo wamo, huua watu 600 kwa mwaka.

Anaangamiza idadi hiyo licha licha ya kwamba ni mnyama hatari zaidi na  hodari duniani kutokana na ukubwa wake.

Anaweza kuwashambulia wanadamu kwa njia mbalimbali. Kwa kawaida huwaua kwa kuwakanyaga. Kwa vile tembo wa Afrika anaweza kuwa na uzito wa tani nnne lakini wale wa Asia hadi tani tano na nusu.

Tembo pia anaweza kutumia mkonga wake kuwaburuza na kuwatupa wanadamu mbali kisha kuwavunjavunja akiwakanyaga chini ardhini. Inawezekana pia, kwa tembo kupiga watu kwa kutumia meno na kuwaumiza hata kuua. 

Viboko huua watu 500 kwa mwaka. Wapo kwenye orodha hii kutokana na kuwa wala nyasi, lakini kiasili ni mojawapo ya wanyama hatari zaidi duniani.

Viboko hutumia meno yenye ncha kali karibu nusu mita kupigana na kuuma kiumbe, kukata mwili wa mwanadamu katikati. Anauma kwa nguvu karibu mara tatu ya simba.

Wakiwa katika eneo lao, viboko wanaweza kushambulia binadamu anapokaribia makazi yake na wanajulikana kushambulia boti ili kujilinda wakifananisha na wanyama wanaowinda. Kiboko anajulikana kula wanyama wa aina yake kutokana na kukata tamaa.

Simba naye yupo anatajwa kuwa ni mwamba wa porini, ambaye anaishi mbugani ni mwindaji mkali 

hushambulia wakati wa usiku kwa kutumia makucha makali na kusababisha majeraha makubwa na kwa kuuma na kung'ata mifupa na fuvu la kichwa.

BBC