Wanafunzi watakiwa kujali jitihada za serikali kwa kufaulu vizuri

By Elizabeth John , Nipashe
Published at 07:52 AM Apr 28 2024
MKUU wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi.
PICHA: ELIZABETH JOHN
MKUU wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi.

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kujali jitihada za serikali katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwa kufaulu vizuri masomo yao.

Mtaka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mount Kipengere wilayani Wanging'ombe alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya elimu pamoja na kuwatakia kheri kwanafunzi wa kidato cha sita wakitarajia kufanya mtihani wao wa mwisho hapo mei 6 mwaka huu.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe, Nicephorus Mgaya amesema serikali imepeleka fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni shuleni ili wanafunzi wasome katika mazingira rafiki.

Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta ametaka kuona matokeo chanya katika elimu kwa wanafunzi hao kupitia uwekezaji wa miundombinu hiyo ya elimu.

Baadhi ya wanafunzi hao akiwemo Matrida Nziku na Joseph Mapunda wamekiri kuwapo kujengwa kwa miundombinu rafiki shuleni hapo na inawasaidia kusoma katika mazingira mazuri yatakayowawezesha kufanya vyema katika masomo.