Rais Samia kufanya ziara Tanga

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 05:13 PM Feb 12 2025
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dk. Batilda Burian
Picha: Mtandao
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dk. Batilda Burian

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dk. Batilda Burian, amesema ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan, itaanza Februaru 23, mwaka huu, kwa kukagua na kuzindua miradi mitatu mikubwa.

Dk. Batilda ameyasema hayo leo, katika kikao na viongozi wa dini, vyama vya siasa, viongozi wa bodaboda na wafanyabiashara.

Amesema miongoni mwa miradi atakayo tembelea ni pamoja na Bandari ya Tanga, mradi wa umwagiliaji, shule ya mchepuo wa sayansi kwa wasichana na kuweka mawe ya msingi katika Bomba la Mafuta.

Pia kufika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Tanga na wa umwagiliaji wenye thamani ya Sh. billioni 18 ulioko Wilayani Korogwe.

Kiongozi huyo, amesema baada ya hatua hizo, atatembelea kila wilaya na kuzungumza na wananchi kisha kufanya mkutano kabla ya kuondoka.

Hii ni ziara ya kwanza mkoani humo tangu Rais Samia aingie madarakani. Aidha, amewataka wananchi wa kujiandaa kumpokea, akisisitiza katika ziara hiyo atasikiliza kero mbalimbali za wananchi.

“Ndani ya miezi mitano bandari tayari imeshatuingizia Sh. billioni 100 hii itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufungua uchumi wa Tanga, pia tayari kazi ya kusanifu barabara kutoka Segera hadi Tanga unafanyika, ili itanuliwe,” alisema Dk. Batlida.