Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kikao na Rais wa China, Xi Jinping wamejadiliana kuimarisha uhusiamo mzuri uliodumu zaidi ya miaka 60.
Rais Samia alikutana na Rais Jinping pamoja na ujumbe wake mapema leo katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing.
Aidha, Rais Samia amefanikiwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na nchi muhimu duniani ikiwepo China tangu alipoingia madarakani mwaka 2021.
Baada ya kikao hicho Rais Samia, Rais Jinping na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, walishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED