BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani, limepitisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2025/2026 ya Sh. bil. 60 ambayo ni ongezeko la asilimia 5.7 ukilinganisha na bajeti ya 2024/2025.
Kadhalika, halmashauri hiyo inatarajia kutumia Sh. mil. 450, kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mafuta, fedha zinazotokana na mapato ya ndani.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ramadhani Possi, ameeleza hayo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, amesema fedha hizo ni katika mpango wa bajeti wa 2024/2025.
Possi, amesema fedha kwa ajili ya kituo hicho, zimeshapatikana na sasa wanaendelea na utaratibu wa kumpata mkandarasi kuanza ujenzi.
Kadhalika Mkurugenzi huyo amesema, mbali ya kituo hicho cha mafuta, pia katika bajeti hiyo, kupitia mapato ya ndani, mpango ulikuwa kukusanya Sh. bil. 17 kununua basi.
Amesema mchakato wa manunuzi unaendelea na wanatarajia mwezi ujao basi hilo liwe limeshafika katika halmashauri hiyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED