Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya kutoka Tanzania Dk. Ntuli Kapologwe, ameibuka mshindi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC) na kuwashinda wagombea wengine sita waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Dk. Ntuli anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Prof. Yoswa Dambisya wa Uganda ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo kwa mihula miwili ndani ya miaka 10.
Dk. Ntuli Kapologwe kwa kuzingatia vigezo maalum vilivyowekwa katika makubaliano ya Jumuiya hiyo, ataongoza kwa muda wa miaka mitano.
Akizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la uchaguzi Februari 12, 2025, Waziri wa Afya nchini Tanzania Jenista Mhagama amesema kuwa nafasi hiyo ilipotangazwa kwa mara ya kwanza jumla ya waombaji 47 waliwasilisha wasifu wao na kati yao, saba walichaguliwa kuendelea baada ya mchujo wa awali.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED