Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Bob Wangwe amemtaka Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, kujiuzulu katika nafasi yake kwa kile alichodai kutoa kauli inayokiuka maadili ya uongozi.
Akizungumza na Nipashe, Bob amesema kauli aliyoitoa kiongozi huyo kuhusu kushinda kura nje ya boksi la kura inaonesha utovu wa kimaadili alionao kiongozi huyo.
“Ni kauli ambayo siyo tu inaonesha ni kwa kiasi gani nchi yetu inaongozwa na baadhi ya viongozi wasiokuwa na maadili na hofu ya Mungu bali pia inaonesha jinsi watanzania walivyowavumilivu, inatakiwa ajiuzulu nafasi yake” Bob Wangwe.
Katika kipande cha video kilichosambaa mtandaoni, Waziri Nape amesikika akisema kuna mbinu nyingi za uchaguzi ikiwemo halali na haramu.
“Matokeo ya kura siyo lazima yawe yale ya kwenye boksi ,inategemea nani anahesabu na nani anatangaza” amesikika Waziri Nape katika Video hiyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED