MWANANCHI mmoja aliyefahamika kwa jina la Mkono wa Chuma aliyejifanya kuwa mtumishi wa Wizara ya Ulinzi akijifanya anaweza kuwasaidia wananchi kupata ajira kwenye Jeshi la Ulinzi amekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro.
"Wapo pia wanaowapigia simu wananchi kuwaambia watazifunga laini zao muda wowote na kuwataka wananchi kutoa pesa pia wamekamatwa, jumla ya watuhumiwa 41 simu 41 na laini za simu 88 za mitandao tofauti tofauti zimekamatwa ambazo zimekuwa zikitumika katika utapeli na wizi wa mtandaoni," amesema Kamanda Muliro.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED