Wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kuwafunga miaka 15 Iraq

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:36 PM Apr 28 2024
Bunge la Iraq huko Irbil.
Picha: Christophe Petit Tesson/dpa/picture-alliance
Bunge la Iraq huko Irbil.

BUNGE la Iraq limepitisha muswada unaopinga marufuku mahusiano ya watu wa jinsia moja na adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela. Hatua hiyo imelaaniwa na mashirika ya haki za binadamu na kusema kwamba ni mashambulizi dhidi ya haki za binadamu.

Chini ya muswada huo uliofanyia marekabisho sheria ya kupinga biashara ya kujiuza ya mwaka 1988, watu waliobadili jinsia watafungwa miaka mitatu jela. Muswada uliopita, ulikuwa umependekeza adhabu ya kifo kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Muswada huo unataja kuwa mabadiliko ya jinsia ya kibaiolojia kulingana na tamaa za watu binafsi ni uhalifu na kuwaadhibu watu waliobadili jinsia na madaktari ambao hufanya upasuaji.

Mapenzi ya jinsia ni mwiko katika jamii ya kihafidhina ya Iraq, lakini hapakuwa na sheria ambayo ilitoa adhabu ya wazi dhidi ya watu wanaoshiriki vitendo hivyo.