Papa Francis afanya ziara ya siku moja mjini Venice

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:45 PM Apr 28 2024
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis mjini Venice.
Picha: Alberto Pizzoli/AFP/Getty Images
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis mjini Venice.

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ametembelea mji wa Venice, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya Roma ndani ya kipindi cha miezi 7, kufuatia wasiwasi kuhusu afya ya kiongozi huyo aliye na umri wa miaka 87.

Papa Francis amefanya ziara nyingi duniani katika kipindi cha miaka 11 ya uongozi wake, lakini hajasifiri tangu alipozuru mji wa Ufaransa wa Marseille mnamo mwezi Septemba. Francis, ambaye anatumia kiti cha magurudumu, amepata matatizo ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni, kutokana maumivu ya goti hadi upasuaji wa hernia na utumbo.

Kiongozi huyo alilazimika kusitisha ziara yake ya Dubai mwezi Desemba baada ya kuugua, ambako alitarajiwa kuhutubia hadhara ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi. Akiwa mjini Venice, Papa Francis atalitemebelea gereza la wanawake katika kisiwa cha Giudecca.