KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara.
Dk. Nchimbi ametembelea kaburi hilo leo Julai 28, 2024, pamoja na mambo mengine ametoa pole kwa familia na kuzungumza na wananchi wa Lupaso.
Balozi Nchimbi amesema "Naomba nikiri kuwa mimi ni mwanafunzi wa Hayati Benjamin Mkapa na nimekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa katika kipindi chake kwani ndiye alinilipia ada ya kusoma chuo kikuu, " alisema Dk. Nchimbi.
Amesema: "Hayati Mkapa alikuwa mfuatiliaji sana na alitulea na siyo sisi lakini kwa Watanzania wote aliwalea pia alikuwa mzalendo kwa taifa, alifanya mabadiliko makubwa kwa nchi yake na kwa CCM. Lakini yote CCM chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan. tutaendelea kuyaenzi yale yote aliyoyoacha Hayati Benjamin Mkapa".
Akiwa Kijijini Lupaso, Dk. Nchimbi kwa niaba ya CCM alichangia Sh. milioni 10 kwa ajili ya kuanza kukarabati shule iliyopo kjijini hapo.
Katika ziara hiyo Dk.Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni, Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED