CHADEMA Korogwe vijijini, yapata mwenyekiti mpya

By Elizabeth Zaya , Nipashe Jumapili
Published at 05:41 PM Nov 10 2024
CHADEMA Korogwe vijijini, yapata mwenyekiti mpya
Picha: Mtandao
CHADEMA Korogwe vijijini, yapata mwenyekiti mpya

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Korogwe vijijini, kimefanya uchaguzi katika nafasi mbalimbali ndani ya chama na mabaraza yake.

Katika uchaguzi huo, Oliver Kisaka ameibuka mshindi katika nafasi ya Uenyekiti kwa kupata kura 53 dhidi ya 33 alizopata mpinzani wake, Salimu Sempoli.

Kwa nafasi ya Katibu, aliyeshinda ni Thomas Lwoga, aliyepata kura 48 dhidi ya 39 alizopata Lucyana Andrea, nafasi ya Mwenezi ameshinda Ibrahim Wiss kwa kura 44, dhidi ya Rajabu Magogo aliyepata kura 41 wakati katika nafasi ya Mhazini, ameshinda Twaha juma kwa kura 50 dhidi ya Hemedi Alex ambaye amepata kura 37.

Kwa nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu, aliyeshinda ni Jumanne Billa kwa kura 68 dhidi ya Aulelian Nziku aliyepata kura 18, nafasi ya mjumbe ameshinda Ramadhani Kihiyo kwa kupigiwa kura za ndiyo 81 na za hapana sita.

Baraza la Wazee, ameshinda Josiah Tumaini kwa kura 22, Makamu Mwenyekiti ni Jalali Njenga kwa kura 17, Said Daffa kura 23 katika nafasi ya utunza hazina, Naibu Katibu mkuu ameshinda Athuman Ndiga kwa kura 21, wakati nafasi ya Katibu ameshinda Ally Mtangi kwa kura 19.

Baraza la Wanawake(BAWACHA), ameshinda Aminata Saguti kwa kura 11, nafasi ya Katibu ni Mwajuma Abdallah kura 13, Mratibu wa Uenezi ameshinda Angelina Mhina kwa kura 15, Mhazini ni Ester Dastani kwa kura 11.


Baraza la Vijana (BAVICHA), Mwenyekiti ameshinda George Shafi kwa kura 13, Katibu ni Kaimu Yahya,kura 13, Katibu Mwenezi ni Msumari Kembo kwa kura 13 na Mhazini ni Adinani Mwalimu kwa kura 13.