Shambulizi la Israel laua watu 20 Gaza

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:02 PM May 19 2024
Mapambano yakiendelea Ukanda wa Gaza.
Picha: -/AFP
Mapambano yakiendelea Ukanda wa Gaza.

HOSPITALI moja huko Ukanda wa Gaza imesema shambulizi la anga lililofanywa na Israeli lililoilenga kambi moja ya wakimbizi katikati mwa eneo hilo la Palestina limewaua watu wasiopungua 20.

Taarifa ya hospitali hiyo ya Mashahidi wa Al-Aqsa imesema imepokea miili ya watu 20 na wengine kadhaa waliojeruhiwa baada ya ndege za Israel kuilenga nyumba moja kwenye kambi ya wakimbizi ya Al-Nuseirat katikati mwa Gaza.

DW imeandika kuwa, Mashahidi wamesema shambulizi hilo limetokea mnamo saa tisa za usiku. Jeshi la Israel limesema linachunguza taarifa hizo.

Mapambano makali na mashambulizi mazito ya Israel yamekuwa yakiripotiwa kwenye kambi hiyo tangu Israel ilipoanzisha oparesheni yake ya kijeshi kwenye mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah.

Wanamgambo wa Kipalestina wamekuwa wakipambana na vikosi vya israel kwenye kambi nyingine ya Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.