‘Serikali imesikia kilio chenu, fungueni maduka’

By Dotto Charles , Nipashe
Published at 02:53 PM Jun 25 2024
MWENYEKITI Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Massawe.
Picha: Maktaba
MWENYEKITI Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Massawe.

MWENYEKITI Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Massawe, amesema kuwa TRA imekubali kuboresha mfumo wake wa forodha na hivyo kamata kamata ya wafanyabiashara haitokuwepo tena, na kuwaomba wafanyabiashara wote waliofunga maduka wayafungue kwani serikali tayari imeshasikia kilio chao.

Massawe amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa Habari, huku akiwatoa hofu wafanyabiashara hao kuwa makubaliano hayo waliyoyaweka ni ya muda mrefu.

Pamoja na hayo, Massawe amewataka wafanyabiashara hao kuitii Serikali “Tumefunga maduka ili kupaza sauti Serikali imetusikia, pia tuonyeshe nidhamu kwa mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan, kwasababu yote yaliyofanyika ni kwa juhudi zake. Kwa faida yetu tufungue maduka tufanye biashara changamoto tulizozipeleka hazitajirudia tena” amesema.