RC Makonda atembelea mradi mkubwa wa maji Ngorongoro

By Beatrice Shayo , Nipashe
Published at 11:51 PM Jul 03 2024
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda atembelea mradi mkubwa wa maji Ngorongoro.
Picha: Beatrice Shayo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda atembelea mradi mkubwa wa maji Ngorongoro.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amekagua mradi mkubwa wa maji na uchimbaji wa visima virefu vya maji katika Wilaya ya Ngorongoro jijini Arusha.

Mradi huo mkubwa wa maji unatekelezwa baina ya Tanzania na Dubai inayoongozwa na Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, mtawala wa Dubai na makamu wa Rais wa milki za kiarabu (UAE) ukiwa na malengo ya kuchimba visima virefu 37.

"Leo tunakuja kuwaambia kuwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Mwanadiplomasia namba moja, Mkuu wa nchi yetu na Rais wetu ametujengea mahusiano mazuri na nchi za Falme za kiarabu na sisi wana Ngorongoro tumeanza kuyaona matunda hayo ikiwa ni ndoto na shauku ya Makamu wa Rais Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.", amesema Makonda.

1
Makonda amesema hadi sasa jumla ya visima 18 vimeshachimbwa kwenye vijiji mbalimbali na 12 vimeshakamilika na wananchi wameanza kunufaika na huduma ya maji.
2