KATIBU wa NEC,Itikadi,Uenezi na Mafunzo,Amos Makalla,amesema CCM itahakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki.
Aidha,amesema chama hicho kina mtaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 hivyo hakihitaji kubebwa bali kinaalama kila mahali ambazo ni mtaji.
Akizungumza jana na wananchi wa Monduli katika mji wa Mto wa Mbu, alisema uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 27,mwaka huu utakuwa ni uwanja sawa kwa kila mmoja ambapo wananchi wataamua kiongozi wanayemtaka.
"CCM ni chama kiongozi,tunawahakikishia uchaguzi huru na haki,mgombea atakayeshinda ndiye atakayetangazwa.Sisi hatuna wasiwasi maana tumefanyakazi nzuri inajieleza yenyewe,"amesema.
Aidha,aliwataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wakazi kuanzia Septemba 11 hadi 20,mwaka huu ili wawe na sifa ya kuchaguzi viongozi wa vitongoji,mitaa na vijiji.
Aidha,alisema ni muhimu wananchi wakawachagua viongozi wa CCM katika ngazi zote huku akiwa na imani kuwa Monduli ni kijani (CCM).
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED