MKUU wa Kanisa Katoliki, Papa Francis,amewatawadha makadinali 20 ambao wataongezwa katika orodha ya kupata mrithi wake baada ya kifo au kujiuzulu.
Miongoni mwa waliotawazwa wakati wa hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye kanisa ya St Peter Basillica, 16 miongoni mwao walikuwa na umri wa chini ya miaka 80, ikiwa na maana kwamba wanaweza kushiriki katika kumchagua Papa mpya.
Wakati akichagua makadinali hao,Papa Francis alionyesha kuzingatia wale pia kutoka jamii za pembezoni.
Miongoni mwa waliochaguliwa ni askofu Peter Ebere Okapaleke mwenye umri wa miaka 59 kutoka Nigeria.
Askofu Mkuu Hyderabad Anthony Poola mwenye umri wa miaka 60 ni wa kwanza kuchaguliwa kutoka kwenye jamii yenye hadhi ya chini zaidi nchini India.
Pamoja na makadinali hao 20 wapya, Papa Francis mwenye umri wa miaka 85 sasa ameteua jumla ya makundi manane ya makadinali 83 kutoka jumla ya 132 wenye umri wa kujiunga kwenye kundi la kuchagua mkuu mpya wa kanisa.
Chanzo:DW
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED