Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wa taasisi mbili za Serikali.
Taarifa iliyotolewa na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu leo May 6, 2024; imewataja walioteuliwa, kuwa ni Dk Elirehema Doriye na Christopher Kadio.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Dk Doriye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), ambapo imeelezwa kuwa, aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Aidha, taarifa hiyo toka Ikulu, imesema Rais Samia amemteua Kadio kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Taarifa hiyo imesema kuwa Kadio anachukua nafasi ya Esther Lugwisha, ambaye amemaliza muda wake.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED