Viongozi wa Ulaya kukutana kwa dharura kuijadili Ukraine

By Enock Charles , Nipashe
Published at 01:54 PM Feb 16 2025
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz
PICHA:MTANDAO
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz

Viongozi wa mataifa ya Ulaya wameitisha mkutano wa dharura mjini Paris nchini Ufaransa wiki ijayo ili kujadili hatma ya vita vya Ukraine ikiwa ni chini ya miezi miwili tangu kuingia kwa Donald Trump madarakani.

Uongozi wa Trump umeiacha Ukraine katika sintofahamu baada ya rais huyo kukatisha msaada wa silaha kwa nchi hiyo na kuahidi kumaliza vita hivyo kwa njia ya mazungumzo. 

 Upande wa Trump ulisema viongozi wa Ulaya watashauriwa lakini hawatashiriki katika mazungumzo yoyote kati ya Marekani na Urusi kuhusu kumaliza vita hivyo.

 Viongozi wa Ulaya wanatazamiwa kukutana wiki ijayo kwa mkutano wa dharura kuhusu vita nchini Ukraine, kujibu wasiwasi wa kwamba Marekani inaendelea kuhusisha Urusi pekee katika mazungumzo ya amani hatua ambayo itafungia bara hilo nje.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer ambaye anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa kilele huko Paris, alisema “ni kipindi nadra sana kwa usalama wetu wa kitaifa na ni wazi Ulaya lazima ichukue jukumu kubwa katika Nato.”

Haya yanajiri baada ya mjumbe maalum wa Donald Trump nchini Ukraine kusema viongozi wa Ulaya watashauriwa lakini hawatashiriki katika mazungumzo yoyote kati ya Marekani na Urusi kuhusu kumaliza vita.

Viongozi wakuu wa Ikulu ya White House, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, wanatarajiwa kukutana na wapatanishi wa Urusi nchini Saudi Arabia katika siku zijazo.

CHANZO: MTANDAO