Rais Samia apiga simu pambano la KO ya Mama, awapa neno mabondia Watanzania

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:59 PM Dec 26 2024
Rais Samia apiga simu pambano la  KO ya  Mama, awapa neno mabondia Watanzania
Picha: Mpigapicha Wetu
Rais Samia apiga simu pambano la KO ya Mama, awapa neno mabondia Watanzania

Rais Samia Suluhu Hassan amepiga simu kwenye pambano la KnockoutYaMama (KO ya Mama) na kuwapa salamu za Sikukuu ya Krismasi na kuwatakia mwaka mpya mwema mashabiki waliofurika kwenye ukumbi wa The Super Dome, Masaki kushuhudia pambano hilo.

Katika salamu zake,  Rais  Samia pia aliwataka mabondia Watanzania kupambana na kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.

Katika salamu zake kwa mamia ya mashabiki wa ndondi na mabondia ukumbini hapo, Rais Samia ambaye alieleza kulifuatilia pambano hilo  laivu amesema, kilichompa hamasa ni jina la mchezo la Knock Out ya Mama.

"Wosia wangu mcheze vizuri, sheria zifuatwe," amesema Rais Samia alipokuwa akizungumza na mashabiki ukumbini hapo ambao muda wote walikuwa wakimshangilia.

Awali,  Rais alianza kwa kumtania Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni mgeni rasmi  na kumueleza alikuwa na wasiwasi wasimweke yeye Waziri mkuu ulingoni, utani ulioamsha shangwe kwa  mashabiki huku waziri  mkuu pia akitania kwamba amewahi kuwa bondia.

Pia amewasihi Mabondia wa Kitanzania kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mapambano yao .

1