Mwandishi Nipashe achaguliwa Mwenyekiti Soka la wanawake

By Shufaa Lyimo , Nipashe Jumapili
Published at 10:41 AM Sep 15 2024
Somoe Ng’itu akila kiapo.
Picha: Mpigapicha Wetu
Somoe Ng’itu akila kiapo.

MWANDISHI Mwandamizi wa Michezo kwenye gazeti la Nipashe, Somoe Ng’itu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (TWFA) katika uchaguzi uliofanyika jana Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mbali na Somoe, mwanahabari mwingine mwandamizi, Zena Chande wa gazeti HabariLEO alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Somoe alipata kura 37 na mpinzani wake Amina Karuma alipata kura 14,  Zena alipata kura 34 na wapinzani wake Fatuma Seleman alipata kura tisa na Veronica Samo alipata kura nane.

Katika nafasi ya wajumbe wa Kamati ya utendaji, Irene Ishengoma, Ndinagwe Sungura walipita bila kupingwa baada ya Mwanaheri Kalolo kujitoa siku ya uchaguzi.

Baada ya Somoe kutangazwa na kuapishwa, alimteua Beatrice Mgaya kuwa Makamu Mwenyekiti na Hamisa Katambi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA. 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo, Benjamin Kalume baada ya kutangaza matokeo aliwataka viongozi hao wakafanye kazi kwa ushirikiano na kuvunja kambi kwani uchaguzi umemalizika.