Waziri Ndejembi atoa mwezi mmoja kituo cha afya kianze kazi

By Shaban Njia , Nipashe Jumapili
Published at 06:35 PM Oct 06 2024
Waziri Ndejembi atoa mwezi mmoja kituo cha afya kianze kazi
Picha:Mpigapicha Wetu
Waziri Ndejembi atoa mwezi mmoja kituo cha afya kianze kazi

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi ametoa mwezi mmoja Kituo cha Afya Segese kianze kufanya kazi mara moja baada ya kukamilika na kuwa na baadhi ya vifaa tangu mwaka 2023 hali inayosababisha wananchi kuendelea kukosa huduma za afya ya uzazi na upasuaji.

Ndejembi alitoa kauli hiyo baada ya kukagua na kupata taarifa ya kituo hicho kukamilika tangu mwaka jana na kutoanza kutoa huduma kwa wananchi kwa madai ya kukosa nishati ya umeme, maji pamoja na watoa huduma(Manes Waauguzi).

Amesema, lengo la serikali kutekeleza miradi ya namna hiyo ni kusogeza huduma karibu na wananchi na sio kuwaacha kuendelea kuteseka kwa kufuata huduma za kiafya umbali mrefu na kumtaka Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kituo hicho kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Awali akito ataarifa ya ujenzi wa kituo hicho Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dk. Sisti Mosha ameahidi kutekeleza agizo hilo nakusema ujenzi wake ulianza Oktoba mwaka 2022 na kukamilika mwaka 2023 kwa gharama ya Sh.milioni 470 fedha kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri.

Amesema,kituo kimekamilika na kuwa na majengo ya Wagonjwa wa nje (OPD), Maabara, Upasuaji na Jengo la Mama na Mtoto na kimeshindwa kuanza kutoa huduma kwa sababu ya ukosefu wa nishati ya umeme, maji pamoja na watumishi watakao toa huduma kwa wagonjwa.

Dk. Mosha amesema, kitakapoanza kutoa huduma kitawafilia wagonjwa wa nje 12,000 kwa mwezi, wajawazito 1,260 na upasuaji 600 na hivi karibuni wanatarajia kupata madawaa na kwamijibu wa sensa ya watu na makazi jumpa ya wakazi 36,247 watapata huduma karibu na kuondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu.