VIJANA wafundwe namna ya kuchamgamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2024, Godfrey Mzava,Oktoba 13,2024,wakati akifunga kongamano la vijana Ilemela lililofanyika uwanja wa TBA uliopo Pasiansi Kata ya Kawekamo,wilayani humo,lenye kauli mbiu isemayo"Tunza mazingira,shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu,ambalo limewakutanisha vijana takribani 1,397.
Anaeleza vijana wakitambua fursa hizo wakizikamata na kuzifanyia kazi,watajenga uchumi wao binafsi na waweze kujitegemea,pia waweze kutoa mchango kwa taifa hivyo Halmashauri hiyo imetakiwa kufanya makongamano ya vijana mara nne,ili kuwajengea uwezo na kutambua fursa zilizopo.
"Hayo ndiyo yalikuwa maelekezo ya Mwenge wa Uhuru,ambapo utapita yafanyike makongamano ya vijana.Ili vijana wapate fursa ya kuelezwa kwa kina,masuala ya falsafa ya Mwenge wa Uhuru,historia ya taifa letu wapi tulipotoka,mapiyo yapi tumeyapita na wapi tulipo na tunataka kwenda,na kuangalia maslahi ya taifa,"amesema
Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Amina Bululu,amesema Halmashauri hiyo inafursa mbalimbali ikiwemo ya ardhi ambayo vijana wanaweza kutumia kwa ajili ya kilimo na uwekezaji mbalimbali.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED