MBUNGE wa Hai,mkoani Kilimanjaro, Saashisha Mafuwe,ameshiriki zoezi la uandikishaji katika orodha ya mpiga kura ambalo linaendelea kote nchini.
Saashisha alishiriki zoezi hilo nyumbani kwao alikozaliwa Kijiji cha Uduru, Kata ya Machame Kaskazini.
Baada ya kujiandikisha, Mbunge huyo, amewahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuwa na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyija Novemba 27 mwaka huu.
Zoezi hilo la kujiandikisha lilianza rasmi nchini kote kuanzia Oktoba 11 hadi 20 mwaka, huku rai kubwa ikitolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yao.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED