Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umenyakua tuzo ya mtoa huduma za hifadhi ya jamii kwenye Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini Geita.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Thomas Labi, kwa niaba ya Mfuko, alikabidhiwa tuzo ya mshindi wa pili Katika kundi la Hifadhi na mgeni rasmi Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
PSSSF imetehamisha shughuli zake, ambapo kupitia PSSSF kidigitali, wanachama wanaweza kupata hduuma za mfuko kupitia PSSSF kiganjani na PSSSF Member portal.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED