JAMII imetakiwa kuwapa nafasi watoto wa kike katika kushika hatamu na nafasi mbalimbali za uongozi.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Plan Internationa- Tanzania, Jane Sembuche alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kuelekea kilele cha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka Oktoba 11.
Sembuche alisema: " Ndiyo mama sisi Plan International tumeanzisha kampeni iitwayo Girls takes over ambayo inamwezesha mtoto wa kike kushika hatamu katika jamii pamoja na nafasi mbalimbali katika jamii, pamoja na kampeni ya 'Sikia sauti zetu'"
Alisema mtoto wa kike popote alipo anaweza kushika hatamu kwa yeye kuwa kiongozi inawezekana bali kujiwekea malengo na kujiamini kama anaweza.
Alisema wanakampeni ya 'Sikia sauti zetu' ambayo inamwezesha mtoto wa kike kusikilizwa changamoto zinazowakabili kiweno washike nafasi katika uongozi.
Alisema kwa sasa nchini takwimu zinaonyesha kuna idadi lubwa ya wanafunzi wa kike wanaanza shule na kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
Swmbuche alisema: "Tuboreshe mazingira na elimu tutamwezesha mtoro wa kike kufika mbali kimaendeleo. Huduma ya vyoo shuleni, asitembee umbali mrefu, jamii iruhusu watoro kwenda shule hivi vyote vitasaidia mtoro wa kike kuendelea".
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED