Makalla: Maandamano ya CHADEMA ni kujidhururisha

By Salome Kitomari , Nipashe Jumapili
Published at 12:00 PM Sep 08 2024
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM,Amos Makalla.
Picha: CCM
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM,Amos Makalla.

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM,Amos Makalla ameyakandia maandamano ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), kuwa hayajaleta maendeleo zaidi ilikuwa ni kujidhururisha.

Akizungumza na wananchi wa Monduli katika eneo la Mto wa Mbu, alisema ni muhimu wanachi wakaelewa kuwa maandamano hayajengi shule,zahanati bali ni kupoteza muda.

"Wenzenu wanawaandamanisha wanapata posho nyie mnaandamana bure na kuambiwa mkunje ngumi,CCM inawajibu ni chama kiongozi kitakachowaletea maendeleo.

Alisema CHADEMA haina uwezo wa kushinda uchaguzi bali inapotokea wameshinda ni kwasababu kuna mgogoro ndani ya CCM lakini wenyewe hawawezi.

Januari 24 mwaka huu,CHADEMA walifanya maandamano kuanzia Dar es Saalam,baadaye yakafuata Mbeya,Mwanza na Arusha wakiwa na hoja ya Katiba mpya.

Kuhusu Uchaguzi wa Seikali za Mitaa alisema: "Ni muhimu kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa wachague viongozi wenyeviti wa vitongozi,kijiji,mitaa ambao ni muhimu sana.Matumaini tuliyonayo,fedha za miradi zinapokuja zipate watekelezaji."

Aidha,alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameshisha fedha nyinginza maji,zahanati,shule na kwamba ni muhimu watenge siku moja kati ya Septemba 11 hadi 20,2024 kwenda kujiandikisha ili kupiga kura Novemba 27,2024.

"Wana CCM,mashabuki wa CCM,wasio na vyama ila wapenda maendeleo wajitokeze ili tumoe nguvu Rais Samia ambaye amethibitika ni mzalendo pekee anayeleta maendeleo,kila unapopita kuna alama ya mradi darasa,kituo cha afya mradi wa maji yote yamefanywa na serikali ya CCM,"alisema.

Aidha, alisema ni muhimu vijiji 62 na vitongoji 230 viwe kijani (CCM), na kwamba chama hakitapitisha wagombea ambao itawalazimu kutumia dodoki na sabuni kuwasafisha.