KATIBU wa NEC,Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, amesema kuwa CCM inatambua na kuthamini mchango wa wadau wa maendeleo ndani ya chama huku akiwahakikishia kuwashika mkono na kuwasikiliza.
Kiongozi huyo aliyasema hayo leo Septemba 8,wakati wa kukabidhi vyeti vya shukrani na pongezi kwa wadau 20,vilivyoandaliwa na Kamati ya Siasa Wilaya ya Simanjiro.
Amesema chama kitaendelea kuwashika mkono wadau na kuwasikiliza kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi,na kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho anatambua kazi kubwa wanayoifanya wilayani humo.
Aidha, amesema wadau wakiwa na mazingira mazuri ya kufanyakazi watasaidia upatikanaji wa ajira,watalipa kodi halali na kuongeza mapato ya serikali pamoja na kuongeza uwezo wa serikali kuwahudumia wananchi.
"Cheti hili nilichowakabidhi hakina maana kubwa kulinganisha na mnachokitoa,Ila maneno yaliyopo kwenye cheti kuwa CCM inatambua nchango wenu yana thamani kubwa,"amesema.
"Nawahakikishia CCM itaendelea kushirikiana nanyi kuboresha mazingira ya kufanyabiashara na kama changamoto zipo zitatatuliwa na CCM,"amesema Makalla.
Aidha,amewataka kuendelea kushirikiana na kwmaba kama kunachangamoto wapaze sauti katika mfumo wa chama
"Natambua changamoto zilizopo ikiwamo maji,kituo cha afya tumejipanga kwa ajili ya majibu,nimekuja nimekamilika nina Naibu Waziri wa Madini na Kamisha wa Madini,ambaye atajibu changamoto hizo leo,"amesema na kuongeza;
"Kama msemaji wa chama natamba na kujiaminisha,napata jeuri hii nikiwaona na nyinyi,kwamba tunaenda kwenye uchaguzi basi endeleeni kukishika mkononchama cha mapinduzi ili kishinde uchaguzi na kushirika dola,ili kushika dola lazima uanze na ushidni serikali za mitaa."
Wadau hao wamesaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa shule huku mmojawapo ni bilionea Laizer ambaye anajenga shule kwa fedha zake.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED