Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake ACT-Wazalendo Taifa, Janeth Rithe, amesema kuwa tabia ya Makonda ya kuwadhalilisha wanawake imekuwa ikijirudia na inakuzwa na kulindwa na viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Rithe ametoa kauli hiyo mkoani Tanga wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Soko la Ngamiani Jana
Katika mkutano huo Rithe amekumbusha matukio ya zamani ambapo Makonda alimdhalilisha Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Kinondoni wakati huo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema kama Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM),vingekuwa vinawathamini Wanawake udhalilishaji huo ungekemewa muda mrefu na Wala usingejirudia kama ilivyo sasa
Mwenyekiti wa CCM,ambaye ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, anafumbia macho tabia hizo za Makonda na tafsiri ya haraka tunaweza sema anabariki udhalilishaji huu dhidi ya Wanawake"amesema Rithe
Amesisitiza kuwa viongozi hao wameshindwa kulea vijana wao kwa maadili na hivyo wanastahili lawama. Amehoji hisia za familia ya mwanamke aliyedhalilishwa na Makonda, akisisitiza kuwa wanawake na jamii kwa ujumla wamedhalilishwa.
Amesema Rais Samia hawezi kukwepa lawama hizi Kwa kuwa amezikalia kimya
Kwa kuhitimisha, Rithe amemtaka Makonda kuomba radhi hadharani kwa matendo yake ya udhalilishaji dhidi ya wanawake.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED