VIKOSI vya kutoa msaada wa dharura na uokoaji vimetatizika kufika maeneo ya kaskazini mwa Afghanistan yaliyoathirika na mafuriko yaliosababisha vifo vya mamia ya watu
Katika eneo la Sheikh Jalal, mojawapo ya maeneo yaliyoharibiwa zaidi, AFP imeelezea kuhusu malori ya misaada yaliojaa chakula, magari ya kijeshi, maafisa wa uokoaji na wakaazi wa eneo hilo wakiwa wamekwama katika maeneo ambayo barabara zilikuwa zimesombwa kabisa.
Mohammad Ali Aryanfar, mmoja wa maafisa wa shirika la Uturuki la kutoa msaada wa kibinadamu la Hak linalojaribu kupeleka chakula katika eneo la Burka, amesema wamekuwa barabarani tangu mapema leo lakini wamekwama katika eneo la Sheikh Jalal.
DW imeripoti kuwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani - WFP, lilituma picha kwenye mtandao wa kijamii wa X likionesha mifuko ya unga ikiwa imefungwa kwenye migongo ya punda, na kusema iliwabidi kutafuta njia mbadala ili kufikisha chakula hicho kwa manusura wa mafuriko hayo huko Baghlan.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED