WATU 37 wamefariki dunia na wengine hawajuliani walipo huko Magharibi mwa Indonesia baada ya mvua kubwa kunyesha na volcano baridi kutiririka na kuharibu nyumba, barabara na misikiti.
Mvua za msimu zilizonyesha kwa saa kadhaa na maporomoko makubwa ya matope kutokana na lava baridi kutoka kwenye mlima Marapi yamesababisha mito kuvuka kingo zake na kuingia katika vijiji vya milimani katika Wilaya nne kwenye Jimbo la Magharibi la Sumatra.
DW imeripoti kuwa, mafuriko yamewakumba watu na kuzamisha nyumba zaidi ya 100 na majengo, Msemaji wa Idara ya Taifa ya Majanga Abdul Muhari amesema.
Lava baridi, pia inayojulikana kama Lahar, ni mchanganyiko wa volcano na vijiwe ambavyo vinatiririka kutoka kwenye miteremko ya volcano wakati wa mvua.
Leo mchana waokoaji walitoa miili 19 kutoka kwenye kijiji kilichoathirika vibaya sana cha Canduang katika wilaya ya Agam na kupata miili mingine tisa katika wilaya jirani ya Tanah Datar, taarifa ya Idara ya Taifa na Utafutaji na Uokoaji imesema.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED