Wateule wa Rais wazingatie viapo utekelezaji wajibu wao
RAIS Samia Suluhu Hassan juzi aliwaapisha viongozi kadhaa aliowateua hivi karibuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa majukumu mapya waliyopangiwa. Viongozi hao ni mawaziri, naibu mawaziri, katibu mkuu wa wizara na makatibu tawala.