Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman (kulia), akisalimiana na viongozi wa chama hicho baada ya kuwasili Dar es Salaam, kuanza ziara ya siku moja ambapo alitarajiwa kujumuika na wa kijamii.
MPIGAPICHA WETU
Magari yakipita kwenye dimbwi kubwa la maji ya mvua yaliyotuama  katika eneo la Kiziani Kitunda, kutokana na mvua kubwa iliyonyesha, jijini Dar es Salaam juzi.
JUMANNE JUMA
Muuza supu akifanya shughuli zake katika  barabara ya Sewa, Mikocheni kiwandani, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam jana, kitendo ambacho ni hatari kwa usalama wake.
BEATRICE MOSES
Makamu  Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo la Bonde (BDF) ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya  Ngomeni, wilayani Muheza  mkoani Tanga, Fatuma Kweka (katikati), akikabidhi kiti mwendo kwa Ofisa Maendeleo ya jamii wa wilaya hiyo, Stella Kategile.
STEVEN WILLIAM
Wajasariamali wenye asili ya kimasai wakitafuta wateja wa kununua viatu katika eneo la Kitunda, jijini Dar es Salaam juzi.
JUMANNE JUMA
Mzee wa Kanisa la Waadventista Wasabato  Muheza Central, wilayani Muheza mkoani Tanga, John Mdoe (kulia),  akiwakaribisha viongozi wa dini, wakati wa futari aliyoiandaa  nyumbani kwake mtaa wa Mdote juzi.  Wapili (kulia) ni Mchungaji Daud Masindi.
STEVEN WILLIAM