Live updates

Stephen Wasira ateuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara

Frank Monyo
Mwandishi
Stephen Wasira
Picha: CCM
Stephen Wasira
Mwanasiasa mkongwe aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali na CCM, Stephen Wasira ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara).


Wasira ambaye jina lake limewasilishwa mbele ya mkutano mkuu wa CCM unaoendelea jijini Dodoma leo Januari 18, 2025, limepata baraka za Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana aliyetangaza kupumzika miezi mitano iliyopita.


Kinachoendelea sasa jina la Wasira litapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM.

Wanachama Tabora wakiwa Mbashara

Mwandishi Wetu
Mwandishi
news
Picha: Mtandao
Televisheni iliyofungwa ikiomesha tukio la Mkutano Mkuu Maalum WA CCM Dodoma.

Wanachama wa CCM mkoani Tabora wakifuatilia Mbashara Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaondelea jijini Dodoma.