Wanasema hawataki alama peke yake wanataka matuta kwasababu ajali eneo hilo zimekuwa za mara kwa mara zikihusisha magari ya Serikali zikiua wananchi wakiwemo wanafunzi.
Hatimaye wananchi wa Kijiji cha Tabu Hotel waliokuwa wamefunga barabara wameondoa vizuizi na magari yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo,Jabir Makame kuingilia kati na kuwaahidi wananchi kuwa matuta makubwa yatajengwa Kesho Oktoba 25, 2024.
DC Makame amefika eneo la tukio na kuwaomba wananchi kuondoa vizuizi na wamekubali ili magari yapite.
Wanasema hawataki alama peke yake wanataka matuta kwasababu ajali eneo hilo zimekuwa za mara kwa mara zikihusisha magari ya Serikali zikiua wananchi wakiwemo wanafunzi.
Mwanafunzi aliyefariki anaitwa Yulia Samson Difrata mwanafunzi wa KIDATO Cha kwanza katika shule ya Sekondari Chigela, walikuwa watatu wengine wakawahi kurudi nyuma.
WANANCHI wa Kijiji cha Tabu Hotel wamefunga barabara kuu ya Dodoma-Morogoro tangu majira ya saa 11 wakishinikiza kufika Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima baada ya gari ya serikali aina ya Cruzer kumgonga mwanafunzi kwenye kivuko cha watenbea kwa miguu na kusababisha kifo chake na gari husika kukimbia.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED