Lakini Leo Juni 26, 2024 Wafanyabiashara sehemu mbalimbali nchini wameendelea na mgomo kwa kutofungua maduka wakisubiri seeikali kutatua changamoto zao.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Karikaoo, Martin Mbwana amewaachia uamuzi wafanyabiashara wa kufunga ama kufungua maduka yao, baada ya kuwapatia mrejesho wa kile kilichozungumzwa katika kikao baina ya viongozi hao na Serikali.
Wafanyabiashara mkoani Iringa wamefunga maduka yao leo Juni 26/2024 ikiwa ni muendelezo wa mgomo unaofanywa na wafanyabiashara mbalimbali nchini.
ZAIDI ya maduka 500 katika Soko la Manzese pamoja na Soko Kuu la Halmshauri ya Mji Tunduma yaliyopo katikati ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe yamefungwa na kusababisha adha kwa wanunuzi wa bidhaa.
Wafanyabiashara katika eneo la mjini kati jijini Arusha wamefunga maduka yao ikiwa ni mgomo ambao wanaufanya kwa madai mbalimbali ambayo bado hawajayaweka wazi.
Kulingana na baadhi ya Wafanyabiashara hao wanasema jana Juni 25, 2024, vipeperushi vilisambazwa kwenye maduka yao kupitia baadhi ya vijana vikihamasisha kufungwa kwa biashara kwa muda wa siku mbili.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED