Live updates

MATUKIO MBALIMBALI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA NCHI NZIMA

Mwandishi Wetu
Mwandishi
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye foleni ya kupiga kura.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika leo tarehe 27 Novemba, 2024.

Msimamizi wa Uchaguzi Arusha: wagombea msifanye kazi za mawakala

Getrude Mpezya
Mwandishi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Msimamizi wa Uchaguzi, John Kayombo

Rais Samia apiga kura Chamwino, ahimiza amani na demokrasia

Augusta Njoji
Mwandishi
news
Picha:Ikulu
Rais Samia apiga kura Chamwino, ahimiza amani na demokrasia

Rais Samia Suluhu Hassan amepiga kura katika kituo cha Sokoine, Kijiji cha Chamwino Ikulu mkoani Dodoma na kuwahimiza watanzania washiriki ipasavyo na wasivunje amani na matokeo yatolewe kama yanavyosema masanduku ya kura.

Akizungumza leo kituoni hapo, amesema "Nimeona watu ni wengi wamejitokeza, kura hizi ni mtindo wa demokrasia, utamaduni wetu wa kisiasa waende kuufanya kwa salama kwa amani, wasivunje amani yetu."

Rais Samia amesema ni matumaini yake siku ya leo itaisha  salama kwa kuwa hadi sasa mambo yanakwenda vizuri na kwamba matokeo yatolewe kama masanduku yanavyosema.

Mgombea Uenyekiti wa Kitongoji CHADEMA Manyoni auawa kwa kupigwa risasi

Thobias Mwanakatwe
Mwandishi
news
Picha;Mtandao
Mgombea Uenyekiti wa Kitongoji CHADEMA Manyoni auawa kwa kupigwa risasi

MGOMBEA Uenyekiti wa Kitongoji cha Stendi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), George Mohamed, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Amoni Kakwale, amefika eneo la tukio na kuahidi kuwa Jeshi la Polisi litahakikisha linawasaka watuhumiwa  wote waliohusika na mauaji hayo.

Biteko apiga kura Shule ya Msingi Bulangwa Bukombe

Mwandishi Wetu
Mwandishi
news
Picha: Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu
Biteko apiga kura Shule ya Msingi Bulangwa Bukombe

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko akipiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi Bulangwa wilayani Bukombe Novemba 27,2024. 

Wananchi wakitafuta majina yao ili kupiga kura Kunduchi

Miraji Misala
Mpigapicha Wetu
news
Picha:Miraji Misala
Mwananchi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam akitafuta jina ili aweze kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mtaa.

Mwananchi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam akitafuta jina ili aweze kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mtaa.

Naibu Meya Urio apiga kura Kunduchi

Miraji Misala
Mpigapicha Wetu
news
PICHA:MIRAJI MSALA
Diwani wa Kunduchi na Naibu Meya Kinondoni, Michael Urio akipiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mtaa katika eneo Kunduchi Shule, jijini Dar es Salaam leo.

Diwani wa Kunduchi na Naibu Meya Kinondoni, Michael Urio akipiga kura kuchagua viongozi  wa serikali za mtaa katika eneo Kunduchi Shule, jijini Dar es Salaam leo.

DC Mwenda : Tutaheshimu maamuzi ya wananchi kwa kiongozi watakayemchagua

Thobias Mwanakatwe
Mwandishi
news
Picha: Tobias Mwanakatwe
DC Mwenda : Tutaheshimu maamuzi ya wananchi kwa kiongozi watakayemchagua

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda,ameshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kupiga kura katika kituo cha zahanati ya Kiomboi bomani huku akisema serikali itaheshimu maamuzi ya wananchi kwa  kiongozi yeyote atayechaguliwa.

Akizungumza leo (Novemba 27, 2024) baada ya kupiga kura amesema kiongozi atakayechaguliwa na wananchi atakuwa ndo huyo huyo na kamwe serikali haitaweza kubadilisha matokeo  bali itaheshimu maamuzi hasa kwa kuzingatia Tanzania ni nchi ya kidemokrasia.

Mwenda amesema katika wilaya hiyo kuna jumla ya vituo 393 na vyama vyote vyenye wagombea kuna mawakala na kwamba ulinzi umeimarishwa kwenye vituo vya kupigia kula.

Meya Songoro ameshapiga kura kuchagua viongozi serikali za mitaa

Imani Nathaniel
Mwandishi
news
PICHA: IMANI NATHANIEL
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, akipiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Dar es Salaam leo mtaa wa Kambangwa Kata ya Mwananyamara ambako ndio mtaani kwake.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, akipiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Dar es Salaam leo mtaa wa Kambangwa Kata ya Mwananyamara ambako ndio mtaani kwake.

DC Longido apiga kura kuchagua viongozi Serikali za Mitaa

Zanura Mollel
Mwandishi
news
Picha: Ofisi ya DC.
DC Longido apiga kura kuchagua viongozi Serikali za Mitaa

MKUU wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha Salum Kalli ameshiriki katika  zoezi la Kupiga kura kwa uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa wilayani humo.

Chamwino Ikulu: Wakazi wajitokeza kupiga kura za viongozi wa Serikali za Mitaa

Ibrahim Joseph
Mwandishi
news
Picha:Ibrahim Joseph
Chamwino Ikulu: Wakazi wajitokeza kupiga kura za viongozi wa Serikali za Mitaa

Baadhi ya wakazi wa Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo Novemba 27,2024.