Jana, CHADEMA ilifanya uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wake wa kitaifa, ambapo Tundu Lissu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho, na John Heche akachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
KINACHOENDELEA UCHAGUZI CHADEMA: Mbowe ampongeza Lissu
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amempongeza Tundu Lissu na wenzake baada ya kuibuka washindi katika uchaguzi wa chama hicho uliofanyika jana Januari 21,2025 na kuhitimishwa Leo
"Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu"- Freeman Mbowe aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
#MkutanoMkuuCHADEMA #NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA), Tundu Lissu amempendekeza kwa Baraza Kuu la chama hicho, Ali Ibrahim Juma kuwa, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar.
#NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA), Tundu Lissu amempendekeza kwa Baraza Kuu la chama hicho, Dk. Rugemeleza AK Nshala kuwa Mwanasheria Mkuu CHADEMA na Mjumbe Kamati Kuu.
#NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA), Tundu Lissu amempendekeza kwa Baraza Kuu la chama hicho, Godbless Lema kuwa Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA.
Lema alikuwa Wakala wa Lissu katika uchaguzi uliofanyika jana wa kumpata mwenyekiti mpya wa chama hicho.
#NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA), Tundu Lissu amempendekeza kwa Baraza Kuu la chama hicho, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Amani Golangwa kuwa Naibu Katibu Mkuu-Bara.
Baraza Kuu hilo limekutana leo Jumatano, Januari 22, 2025 katika kikao kinachofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Golangwa anachukua nafasi ya Benson Kigaila.
Katika uchaguzi mkuu mwaka 2020 wakati Lissu akiwa mgombea urais, Golangwa alikuwa kampeni meneja wa Lissu.
#NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
Mwenyekiti mpya wa CHADEMA, Tundu Lissu amempendekeza kwa Baraza Kuu la chama hicho, John Mnyika aendelee kuwa Katibu Mkuu.
Baraza Kuu hilo limekutana leo Jumatano, Januari 22, 2025 katika Kikao kinachofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ni baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa uchaguzi uliomchagua Lissu kuwa mwenyekiti akimshinda Freeman Mbowe.
#NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
"Hongera sana kwa ushindi Mh. @TunduALissu hakika huu ni ushindi wa mapambano ya demokrasia. Yako mengi ya kujifunza katika mapambano haya. Kipekee ninakupongeza na kukutakia kheri katika majukumu haya makubwa. Ushindi huu ni ushindi wa @ChademaTz ktk vita ya demokrasia ya kweli na chaguzi huru na za haki. Nampongeza pia Mwenyekiti anayemaliza muda wake mh @freemanmbowetz kwa kukubali matokeo na kumpongeza mshindi huu ni ukomavu Mkubwa wa kisiasa @ACTwazalendo tuko tayari kwa ushirikiano na mapambano ya pamoja kwa demokrasia ya nchi yetu."-Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita
#UchaguziCHADEMA2025 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu) , amempongeza Tundu Lissu kwa kuchaguliwa na Mkutano Mkuu wa CHADEMA Taifa kuongoza chama hicho katika nafasi ya Mwenyekiti taifa.
Sugu ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ambapo pamoja na kumpongeza Lissu pia amempongeza mwenyekiti aliyemaliza muda wake Freeman Mbowe kwa kuongoza chama hicho hadi kilipofikia.
#MkutanoMkuuCHADEMA #NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
#UchaguziCHADEMA2025 Tundu Lissu ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akipata kura akiwashinda 513 (51.5%) wapinzani wake Freeman Mbowe ambaye ameshika nafasi hiyo kwa miaka 21 amepata kura 482 (48.3%) na Odero Odero amepata kura moja tu (0.1%).
#MkutanoMkuuCHADEMA #NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
#UchaguziCHADEMA2025 John Heche ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara akipata kura 577 akiwashinda wapinzani wake Ezekia Wenje aliyepata kura 372 na Mathayo Gekul aliyepata kura 49 tu.
#MkutanoMkuuCHADEMA #NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
Baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, uchaguzi utarudiwa kwa sababu hakuna mgombea aliyefikisha 50% ya kura zilizopigwa hivyo wagombea wawili pekee ambao wamekaribiana ndio watapigiwa kura.
Baada ya hapo kutaanza kutangazwa matokeo yote, matokeo hayawezi kutangazwa mpaka matokeo ya mchakato wa marudio kwa upande wa Zanzibar yakamilike kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.
Watakaopigiwa kura kwenye nafasi hiyo ni;
Said Mzee Said
Said Issa Mohamed
#MkutanoMkuuCHADEMA #NipasheMwangaWaJamii #NipasheDigital
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED