#Updates Vikosi ya uokoaji vinaendelea na kazi ya kuokoa watu waliokwama kwenye kifusi katika ghorofa lililoporomoka Kariakoo leo asubuhi.
Kusoma habari hii zaidi tembelea epaper.ippmedia.com
#NipasheMwangaWaJamii #NipasheHabari
Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi.
Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED