Uteuzi huu na utenguzi ameufanya usiku wa Leo Jumapili Machi 31,2024.
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amemhamisha Kundo Andrea Mathew kutoka kuwa Naibu Waziri Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Daniel Baran Sillo, kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sillo anachukua nafasi ya Jumanne Abdallah Sagini ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria
Mbunge wa Viti Maalum Zainab Athuman Katimba, ameteuliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Anachukua nafasi ya Deogratius John Ndejembi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.
Wakati huo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Evans Alfred Mtambi, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mohamed Mtanda, amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, anachukua nafasi ya Amos Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI Degratius John Ndejembi, ameteuliwa na Rais Dk. Samia Suluhu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Ndejembi anachukua nafasi ya Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kabla ya uteuzi huu Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na anachukua nafasi ya John Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED