Wavu Dodoma waahidi makubwa

21Apr 2017
Renatha Msungu
Nipashe
Wavu Dodoma waahidi makubwa

TIMU za mpira wa wavu za mkoani hapa (wasichana na wavulana) zimeondoka na majigambo ya kufanya vizuri katika mashindano ya Ligi ya Muungano yanayotarajiwa kuanza kesho hadi Aprili 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Chama cha Wavu Dodoma (Doreva), Said Kamsumbile, alisema timu yake ambayo ilishika nafasi nne katika mashindano ya taifa imejiandaa vizuri na inaamini itatwaa ubingwa wa Muungano mwaka huu.

"Msafara wa timu yetu utakuwa na wachezaji 18, kati ya hao wakiwemo wasichana nane, na wavulana 10, tunawaamini nyota wetu ambao walifanya maandalizi kwa muda mrefu," alisema Kamsumbile.

Alisema timu zote zilitakiwa kupeleka wachezaji wenye viwango vya juu kwa sababu michuano hiyo inayoshirikisha timu kutoka Tanzania Bara na Visiwani, itatumika kuchagua timu ya Taifa ya itakayoiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Timu nyingine za Bara zinazotarajiwa kushiriki Ligi ya Muungano ni pamoja na Jeshi Stars, Magereza ambazo zitaleta timu ya wanawake na wanaume pamoja na timu ya mkoa wa Arusha.

Habari Kubwa