SportPesa yampagawisha  shambani mkazi Makambako

01Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
SportPesa yampagawisha  shambani mkazi Makambako

MKAZI wa Makambako mkoani Njombe, Iddi Ndondole, ameeleza namna alivyohisi kuchanganyikiwa kwa furaha mara baada ya kupokea taarifa ya kushinda pikipiki ya matairi matatu aina ya TVS King katika Droo ya 56 ya Promosheni ya Shinda na SportPesa.

Iddi Ndondole (kulia), akikabidhiwa pikipiki ya matairi matatu aina ya TVS King Deluxe na Mtangazaji wa Kipindi cha SHINDA NA SPORTPESA mjini Makambako wiki iliyopita. PICHA: SPORTPESA

Ndondole alikabidhiwa zawadi yake hiyo juzi na mwakilishi wa Kamapuni ya SportPesa Tanzania inayoendesha promosheni hiyo.

Akizungumzia mara baada ya kupokea zawadi hiyo, Ndondole alisema kuwa amefurahishwa na promosheni hiyo ambayo sasa imemfanya aanze mwaka kwa neema.

“Kusema ukweli nilifundishwa kucheza na mjomba wangu anaitwa Brison Pascal haswa kwenye zile hatua za mwazo za kujisajili na baada ya hapo nikawa nacheza mwenyewe tu.

“Mara ya kwanza nilishinda Sh. 5,000 , mara ya pili Sh. 26,000  na mara ya tatu nilishinda Sh. 50,000 kwa kweli siku hiyo nilifurahi sana hadi nikanunua kuku ili mimi na mke wangu tule siku hiyo," alisema Ndondole na kuongeza.

“Siku chache baadaye nikiwa naendelea na safari yangu ya kubashiri nikapigiwa simu na mdada anayeitwa Happyness Wandela akinitaarifu kwamba nimejishindia bajaji aina ya TVS KING kutoka SportPesa, aisee sikuamini kama ni mimi nimeshinda, nilikuwa shambani nalima nikaacha nikawahi nyumbani kwenda kumpa taarifa mke wangu naye nilimkuta anakula, alifurahi sana.”

Alifafanua: “Mimi na familia yangu tutaitumia bajaj hii kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na biashara ili kuendesha maisha yetu.”

Aidha, aliwataka Watanzania wengine kuchangamkia fursa za kupata bajaj kwa kujisajili na SportPesa na kushiriki promosheni yake.

 

Habari Kubwa