Milioni 15 zasubiri washindi Mlimani City

01Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Milioni 15 zasubiri washindi Mlimani City

JUMLA ya Sh. milioni sita zimegawiwa kwa wateja waliofanya manunuzi Mlimani City tangu kuanza kwa promosheni ya fanya Manunuzi Mlimani City na Ushinde ijulikanayo kama “Mlimani City Shopping Fest” -

Mlimani City.

Inayoendelea katika kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya huku Sh. milioni 15 zikitafuta mwenyewe.

 Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Mlimani City, Pastory Mroso, alisema jumla ya wateja 60 mpaka sasa wameshajishindia kila mmoja vocha yenye thamani ya Sh. 100,000 na kwamba wameshafanya droo tatu mpaka sasa na kila droo ikitoa washindi 20.

Mroso alisema: "Ni rahisi sana kushinda, unachotakiwa kufanya ni wewe kuja Mlimani City na kufanya manunuzi kwenye duka lolote na kwa bidhaa yoyote ukitumia kiasi cha Sh. 100,000 au zaidi kisha utapewa kuponi ambayo itakuwezesha moja kwa moja kuingia kwenye droo ya kushindania zawadi ya vocha yenye thamani ya Sh. 100,000 ambayo itakuwezesha kwenda kufanya manunuzi tena duka lolote la ndani ya Mlimani City.

"Wewe ambaye hujashiriki nafasi unayo bado kuna droo mbili mbele njoo ufanye manununuzi Mlimani City katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya na ushinde.

Tunayo droo kubwa ya mwisho ambayo mshindi mmoja atajishindia vocha yenye thamani ya milioni 10 na washindi wengine watano watajishindia vocha yenye thamani ya milioni moja kila mmoja, hivyo jumla Sh. milioni 15, zinatatolewa mwishoni."                

Habari Kubwa