Mbaraka nje wiki tatu Azam

17Jul 2017
Faustine Feliciane
Nipashe
Mbaraka nje wiki tatu Azam

MSHAMBULIAJI mpya wa Azam, Mbaraka Yusuph, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa angalau wiki tatu baada ya kugundulika kusumbuliwa na ngiri.

MSHAMBULIAJI mpya wa Azam, Mbaraka Yusuph.

Daktari Mkuu wa Klabu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, alisema jana kuwa nyota huyo amegundulika na matatizo hayo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa afya nchini Afrika Kusini.

Mbali na Yusuph, pia mshambuliaji chipukizi wa klabu hiyo, Shaaban Chilunda, naye atakuwa nje kwa muda huu baada ya kuumia misuli ya paja.

"Mbaraka amefanyiwa upasuaji Afrika Kusini ili kumaliza tatizo lake, atakuwa nje kwa wiki tatu kuuguza majeraha," alisema Mwankemwa.

Alisema Shaaban alifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Muelmed nchini Afrika Kusini na kugundulika kuchanika nyama za paja.

“Shaaban Idd alipatiwa matibabu katika Hospitali hiyo na atatakiwa kupumzika kwa muda wa wiki tatu na baada ya hapo ataanza mazoezi madogo madogo na kuweza kurejea kwenye ushindani,” alisema Mwankemwa.

Azam imeanza maandalizi ya msimu mpya na kwa mujibu wa Mwankemwa, wachezaji wengine wote wapo vizuri na wanaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Habari Kubwa