Kichuya awapoteza Mzamiru, Mo Ibrahim


11Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kichuya awapoteza Mzamiru, Mo Ibrahim


NI kama Shiza Kichuya amewafunika wachezaji wengine kibao waliowahi kucheza Mtibwa Sugar miaka ya nyuma baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa wakali wachache waliotamba katika kikosi hicho sambamba na magwiji wengine.


Winga wa zamani wa Mtibwa Sugar, Uhuru Selemani, anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika klabu ya Royal Eagles, ametaja kikosi chake bora cha muda wote cha Mtibwa akimjumuisha winga wa sasa wa Simba, Kichuya na nahodha wa timu hiyo, Shaaban Nditi.


Uhuru ambaye aliwahi kuichezea Mtibwa mwanzoni mwa 2009 na kufanikiwa kubeba Kombe la Tusker, alitaja kikosi hicho kuwa ni Peter Manyika, Mecky Maxime, Idrissa Rashid, Cresentius Magori, Salum Swedi, Shaban Nditi, Salhina Mjengwa, Aboubakar Mkangwa, Abdallah Juma, Monja Liseki na Shiza Kichuya.


Winga huyo alisema, “Ninajua kuwa kuna wachezaji wengi wamepita Mtibwa, ila kiukweli hawa nimebahatika kuwafuatilia sana na walikuwa moto enzi zao na wengine ambao wanacheza kwa sasa wana vipaji vizuri na wana uwezo mkubwa.


“Tazama leo hii Mtibwa imemtoa Kichuya ambaye anatamba akiwa na Simba, lakini bado wapo wakali wengine kwenye timu. Kichuya kwangu ni bora zaidi kutokana na uwezo wake wa kushambulia, kufunga na kutengenezea wenzake nafasi.

”
Kikosi cha Uhuru kinawaacha nje nyota wa zamani wa Mtibwa ambao kwa sasa wanauwasha moto kisawasawa wakiibeba timu yao mpya waliyojiunga nayo msimu huu ya Simba, Mzamiru Yasin na Mohamed 'Mo' Ibrahim.


Habari Kubwa