Dida apigwa chini Kikosi kipya cha Taifa Stars

19May 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Dida apigwa chini Kikosi kipya cha Taifa Stars

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 24 ambao wanaunda kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya kujiandaa na fainali za Afrika (COSOFA) dhidi ya Lesotho.

Katika kikosi hicho Mayanga amemjumuisha kwa mara ya kwanza mlinda mlango wa timu ya Yanga Beno Kakolanya.

Aidha, kikosi hicho kina sura ya tofauti kabisa na kile walichokizoea mashabiki wa soka pamoja na watanzania huku kikiongozwa na Nahodha machachari Mbwana Samatta anayekipigia nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk.

Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji wafuatao.

MAKIPA
1.Aishi Manula
2.Beno Kakolanya
3.Said Mohamed

BEKI (WAZUIAJI)
1.Shomar Kapombe
2.Hassani Ramadhani Kessy
3.Mwinyi Haji
4.Mohamed Hussein
5.Salim Abdalah
6.Agrey Moris
7.Abdi Banda
8.Erasto Nyoni

VIUNGO (WACHEZESHAJI)
1.Himid Mao
2.Jonas Mkude
3.Salum Abubakar
4.Said Ndemla
5.Mzamiru Yassin
6.Simon Msuva
7.Farid Musa
8.Shiza Kichuya
9.Thomas Ulimwengu

WASHAMBULIAJI
1.Mbwana Samata
2.Mbaraka Yusuph
3.Ibrahim Hajibu
4.Abdulrahiman Mussa

Habari Kubwa