Ben Pol aachia 'mpini' mpya

08Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Ben Pol aachia 'mpini' mpya

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol, ameachia wimbo mpya, unaokwenda kwa jina la 'Phone, akimshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Mr. Eazi.

Akizungumza na gazeti hili, Pol alisema wimbo huo ameutengeneza katika studio ya One Love Records, iliyopo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji Tiddy Hotter.

Pol alisema ujio wa wimbo huo ni moja ya mipango yake ya mwaka 2017 na ameanza kwa kutoka na huo wa 'Phone'.

Alisema tayari wimbo huo umeanza kusikika kupitia vituo mbalimbali vya radio, huku ujio wa video yake ukiwa njiani.

"Wimbo wa Phone ni moja ya malengo yangu ya mwaka huu na ndiyo ujio wangu wa 2017, naomba wapenzi waupokee na kuusikiliza kila mtu ataelewa nini nimejipanga kupitia mwaka huu,"alisema Pol.

Habari Kubwa