Bajaj 'yamwangukia' fundi seremala

03Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Bajaj 'yamwangukia' fundi seremala

Mshindi wa Droo ya 57 ya Promosheni ya Shinda na SportPesa inayoendeshwa na Kampuni ya SportPesa, Nicholaus Sangu, mkazi wa Makambako, Njombe, ameelezea furaha yake kutoka kumiliki baiskeli hadi pikipiki ya matairi matatu aina ya TVS KING Deluxe.

fundi seremala, Nicholaus Sangu, mkazi wa Makambako, Njombe, akiwa kwenye pikipiki ya matairi matatu aina ya TVS King Deluxe baada ya kukabidhiwa juzi, kufuatia kuibuka mshindi wa Droo ya 57 ya Promosheni ya Shinda na SportPesa. PICHA: SPORTPESA

Akizungumza juu ya ushindi wake juzi, Nicholaus alisema: "Nafikiri ni kama mwezi mmoja na siku kadhaa hivi tangu nimeanza kubashiri kupitia SportPesa, huwa nacheza kupitia *150*87# na kwa siku huwa nacheza mara tatu.

"Kama wiki moja hivi mshindi kutoka Makambako alikabidhiwa bajaji yake, nikamuomba anielekeze jinsi alivyojifunza mpaka kushinda bajaj aina ya TVS King Deluxe," alisema na kuongeza.

"Leo mimi nimeshinda sikuamini maana usafiri ninaomiliki ni baiskeli na ninayoitumia katika kazi yangu ya ufundi seremala.

"Baada ya kushinda mtu wa kwanza kumpa taarifa alikuwa ni mke wangu maana amenivumilia sana kutokana na kazi zangu, hasa ukichukulia kipindi kama hiki kazi si nyingi sana."

Sangu alifafanua: "Napenda kuwaambia vijana wenzangu wajifunze na waanze kubashiri na kampuni ya SportPesa, ili kubadili maisha yao maana kama mnavyoona mimi nimebadili maisha yangu sasa hivi nitakuwa ni na biashara yenye kunipa uhakika wa kutokulala njaa. 

"Uzuri wa SportPesa hauhitaji kusubiri baada ya kuweka ubashiri wako ni wewe tu hata ukiweka simu yako chini ya mto ukiamka kama umeshinda basi utakutana na ujumbe mfupi ukikutaarifu kwamba umeshinda na pesa imeshawekwa kwenye akaunti yako ya SportPesa."

Akizungumza juu ya Promosheni ya Shinda na SportPesa inayoendelea nchini, Mkurugenzi wa Utekelezaji na Utawala, Tarimba Abbas, alisema: "Mpaka sasa tumeshawatangaza washindi 69 kesho tunatarajia kumpata mshindi wa 70, hivyo tutabakia na washindi 30 mpaka kufikia tamati ya shindano hili."

"Ningependa kutoa wito kwa wadau wa michezo na washiriki wa mashindano haya kuwa bajaj aina ya TVS KING hutolewa bila gharama yoyote na mshindi hatotumia kiasi chochote cha pesa mpaka atakapokabidhiwa bajaj yake, lakini kuna baadhi ya watu wanaosadikika kuwa ni matapeli wakiwashawishi watu watume kiasi cha fedha, ili wawasaidie kupata ushindi, watu hao ni matapeli na tunaomba endapo mteja wetu atapokea ujumbe kama huo tafadhali awasaliane na namba zetu za huduma kwa wateja ambazo ni 0764 115 588, 0685 115 588 na 0692 115 588.

Habari Kubwa