Wabuni ‘Master Card’ mpya inayotumia harufu ya vidole

21Apr 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wabuni ‘Master Card’ mpya inayotumia harufu ya vidole

MARA zote imekuwa kawaida mtu anapotumia kadi yake ya kuchukua fedha benki, umakini wake unakuwa kwenye kuficha alama yake ya siri, kwani ndiyo silaha yake kubwa katika kulinda usalama wa fedha zake kwenye akaunti.

Sehemu yenye mstari ndio inaonyesha sehemu ya kugusa vidole kwenye ATM.

Hata silaha kubwa ya kiteknolojia iliyopo sasa ni kwamba, namba ya siri ndiyo ama inamruhusu au kumzuia mchukuaji wa fedha kufanikisha lengo.

Wezi wa fedha hao wanatumia ujanja wa uelewa wao katika teknolojia na kuiba fedha kutoka kwenye akaunti mbalimbali ndani ya nchi na hata kimataifa,
Katika ulingo wa kimataifa, zimekuwa zikitumika kadi za kimataifa au ‘master card’ kuiba fedha katika akaunti za watu mbalimbali duniani, huku wenye akaunti na benki nazo zikichukua juhudi zenye hatua mbalimbali za kujihami.

Wabunifu wa vifaa hivyo, hilo kwao limekuwa likiwapa shida na kuwaumiza kisaikolijia, kuhusu ubora wa bidhaa zao na usalama biashara, kuanzia kwao hadi kwa wateja.

Sasa kuna maendeleo mapya ya kiteknolojia yamefikiwa kwamba zimeundwa kadi mpya za kuchukua fedha benki ambazo pamoja na vigezo vyote vilivyopo, pia zinabeba hisia za vidole vya mmiliki wa akaunti.

Hiyo maana yake ni kwamba, mtu mwingine hata akiwa na vigezo vyote, hana nafasi ya kuiba fedha kama alivyolenga na tayari yamefanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini na yameonyesha mafanikio ya kuridhisha.

Ni teknolojia inayotumiwa kwenye ‘Master card’ ikiwa na namna ya kudhibiti wizi wa kimataifa

Mtaalamu wake, Ajay Bhalla, anasema kuna namna inavyowekwa mtu anapitisha vidole kupata ukweli au taarifa ya jambo, huku mtaalamu mwingine, Karsten Nohl, anasema kuna mbadala wa mtu hata akatumia kitu chochote alichokigusa awali kama vile glasi na kupata utambuzi wake.

Pia, utaalamu huo umeandaa mbadala wa aina tisa, iwapo utambuzi utaleta shida, kabla ya kufanya mbadiliko ya alama.

Kwa mtazamo wa jumla wanasema kwamba, hivi sasa matumizi hayo ya alama mpya ni bora zaidi, ikilinganishwa na kutegemea ‘password’ pekee.

"Alama ya vidole imetusaidia kuepuka matumizi ya ‘passwords’ tuliyozoea,” wanaongeza wataalamu hao na vifaa hivyo vinafanya utambuzi kwa pamoja.
L Makala hii ni kwa mujibu wa taarifa mtandao.

Habari Kubwa