Unakumbuka simanzi ya Mv Bukoba?

23May 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Unakumbuka simanzi ya Mv Bukoba?

JUZI ilikuwa kumbukumbu ya tukio la kuzama meli ya MV Bukoba, mwaka 1996. Ni janga lenye vifo vilivyoishitua nchi.

Meli ya MV Bukoba, iliyozama. PICHA: MTANDAO.

Baada ya muda mfupi, iliundwa Tume chini ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali hiyo ya meli iliyopakia abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37.

Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana. 

Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa serikali huongozana na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga,kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu. 

Serikali ilimshitaki aliyekuwa nahodha wa MV Bukoba, Jumanne Rume-Mwiru, (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert Mokiwa; aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo na aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.

 

Katika kesi ya mwaka 1998 katika Mahakama, watuhumiwa walishinda na kuachiwa huru.